Follow by Email

Tuesday, January 13, 2015

Balozi Kilumanga ashiriki Hafla ya kuwakumbuka Wahanga wa shambulizi la kigaidi UfaransaBalozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Chabaka Kilumanga akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa katika Ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo, jijini Paris, Ufaransa. Kitabu cha maombolezo kimefunguliwa kwenye ubalozi wa Ufaransa nchini Comoro na kusainiwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na watu Mashuhuri. 
Balozi Chabaka Kilumanga, akisalimiana na viongozi wa Serikali ya Comoro katika maombolezo hayo.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.