Follow by Email

Monday, December 15, 2014

TANZANIA YAISHAURI ICC KUBORESHA UHUSIANO WAKE NA AFRIKA

Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC). Mkutano huo wa wiki mbili unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya wajumbe wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai wakimsikiliza Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huo, Balozi Irene Kasyanju ambaye katika hotuba yake pamoja na mambo mengine ameishauri Mahakama hiyo kuimarisha uhusiano wake na Afrika.


Na Mwandishi Maalum, New York

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  imesema, mafanikio ya  Mahakama ya Kimataifa ya  Makosa ya  Jinai (ICC) yatategemea  uimarishishwaji wa ushirikiano kati ya  Makahama hiyo na Afrika.

Na kwa sababu hiyo, Tanzania imeshauri kuwa Rais Mpya wa Mkutano wa Nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai hana budi kuhakikisha kuwa moja ya vipaumbele vyake vijielekeze katika kuimarisha uhusiano wa  Makahama hiyo na Afrika.
Ushauri huo umetolewa na Balozi Irene Kasyanju,  Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Sheria, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati akizungumza katika  mkutano wa kumi na tatu wa  Nchi  wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.

Amesema Tanzania ina imani kubwa na Rais mpya wa Mkutano wa Nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Bw. Sidiki Kaba, kutoka Senegal, kuwa afanye kila awezalo katika kuimarisha uhusiano huo ambao kwa sasa  umezorota.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.