Follow by Email

Saturday, December 20, 2014

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa tarehe 21 Desemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Mhe. Zuma atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Zuma atakutana kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 22 Desemba, 2014 kabla ya kuondoka nchini na kurejea nchini kwake.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.


20 DESEMBA, 2014

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.