Follow by Email

Monday, December 22, 2014

Rais Zuma awasili nchini kwa ziara ya kikazi

Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam usiku wa tarehe 21 Desemba, 2014. Mhe. Zuma yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 22 Desemba, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa tayari kumpokea Mhe. Zuma alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Zuma akipokelewa na Mhe. Dkt. Bilal mara baada ya kuwasili nchini. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Maharage
Mhe. Zuma akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye alikuwepo uwanjani hapo kwa mapokezi
Mhe. Rais Zuma akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala wakati wa  mapokezi yake.
Rais Zuma kwa pamoja na Dkt. Bilal wakifurahia burudani ya ngoma iliyokuwa ikitolewa na moja vikundi vilivyokuwepo Uwanjani hapo wakati wa mapokezi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.