Follow by Email

Wednesday, December 24, 2014

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani awasilisha Hati za Utambulisho kwa Papa Francis

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani,  Mhe. Philip Sang'ka Marmo, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francis, Vatican-Roma, Italia. Balozi Marmo anawakilisha Ujerumani na ndiye anayemwakilisha Mheshimiwa Rais kwa Baba Mtakatifu (Holy See). Kwa utaratibu Mabalozi waliopo Italia hawaruhusiwi kuwakilisha nchi zao kwa Baba Mtakatifu yaani Holy See. Nchi nyingine ambazo Mhe. Balozi Marmo anawakilisha ni Austria, Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Hungaria,Ujerumani, Poland, Slovakia, Romania na Switzerland.
Balozi Marmo akiwa katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Francis
Baba Mtakatifu Francis akimsalimia Mtoto wa Mmoja wa Maafisa walioambatana na Balozi Marmo
Baba Mtakatifu Francis akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi waliowasilisha Hati zao za utambulisho, kulia kwa Baba Mtakatifu ni Balozi Philip Marmo na kushoto kwa Baba Mtakatifu ni Mke wa Balozi Marmo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.