Follow by Email

Saturday, November 15, 2014

Waziri wa Uchukuzi akutana na Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harrisson Mwakyembe (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo ofisini kwa Bw. Omar Mjenga, Konseli Mkuu wa Tanzania, Dubai.

 Konseli Mkuu amemueleza Mhe. Mwakyembe kuhusu mazungumzo yake pamoja na Mhe. Gaith  Alghaith, Mtendaji Ma wa Shirika la Ndege la FlyDubai, kuhusu mpango wa shirika hilo kuingia makubaliano ya ushirikiano pamoja na shirika la Ndege la Tanzania(Air Tanzania) ambako Flydubai watatoa ndege tano zitakazochukua njia za ndani (domestic routes) na zile za kikanda (regional routes).

Ushirikiano huu utasaidia kufufua njia zote za ATC na kuiwezesha ATC kuanza kupata mapato.
Njia za kikanda ni pamoja na Kinshasa, Lubumbashi, Goma, Kigali, Bunjumbura, Entebe, Nairobi, Sychelles, Moroni, Madagascar, Mauritius, Maputo, Lilongwe, Lusaka, Joharnessburg, na Harare.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.