Follow by Email

Tuesday, November 4, 2014

Waziri Membe amuaga Balozi wa Qatar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Mhe. Bernard  K. Membe (Mb.) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa kwanza wa Qatar nchini Tanzania Mhe. Jassim M. Al-Darwish alipokwenda kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Waziri Membe akizungumza jambo na Balozi Jassim M. Al-Darwish huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (kushoto) akisikiliza.
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Batholomeo Jungu akisikiliza mazungumzo kati ya Waziri Membe na Balozi Al- Darwish ambao hawapo pichani

--------------Hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Quatar Mhe. Jassim M. Al-Darwish, kwenye Hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje  kwa ajili ya kumuaga Balozi Al-Darwish ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Sehemu ya Wajumbe kutoka Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ubalozi wa Qatar wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga pamoja na wageni wengine waalikwa wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Al-Darwish wa Qatar ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Balozi Jassim M. Al-Darwish akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kumuaga ambapo alitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na kuomba ushirikiano huo uendelee.
Sehemu ya Wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Qatar akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya (wa pili kulia) wakimsikiliza Balozi huyo (hayupo pichani) alipowahutubia.

Waziri  Membe (Mb.) akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa Tembo  Balozi wa Kwanza wa Quatar nchini Tanzania Mhe.  Al-Darwish wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi huyo ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. 
Picha ya Pamoja. 

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.