Follow by Email

Thursday, November 6, 2014

Naibu Waziri afanya ziara ya kikazi nchini Ufaransa


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungungumza na Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, Bw. Jean Christophe Belliard wakati wa ziara yake ya kikazi nchini humo.
Mhe. Dkt. Maalim (katikati)  akiwa na Mhe. Begum Taj (kulia), Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa wakati wa mkutano wao na Bw. Arnaud de Lamotte, Makamu wa Rais wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa na Huduma za Serikali wa Ufaransa wakati wa ziara yake ya kikazi nchini humo.
Mhe. Dkt. Maalim akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa MEDEF-International, Bw. Phillippe Gautier Taasisi ambayo imeandaa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Ufaransa litakalofanyika Paris, Ufaransa mwezi Desemba, 2014.  
Mhe. Dkt. Maalim katika picha ya pamoja na Balozi Taj (wa pili kulia) na Bw. Chiristophe Gallean, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Starch of Tanzania. Mhe. Dkt. Maalim yupo nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Dkt. Maalim (mwenye tai nyekundu) na Mhe. Balozi Taj (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi mbele ya jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.