Follow by Email

Friday, November 7, 2014

Mhe. Rais awaapisha Balozi Zoka na Balozi Shelukindo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha na kumkabidhi vitendea kazi Mhe. Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Mhe Jack Mugendi Zoka
 Mhe. Rais Kikwete akimuapisha Bw. Samwel William Shelukindo kuwa Balozi na Mshauri wa Rais masuala ya Diplomasia  Ikulu Jijini Dar es salaam. Kabla ya uteuzi huu, Balozi Shelukindo alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Balozi Samwel William Shelukindo.
Picha ya pamoja ya Mhe. Rais na Balozi Shelukindo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sfue pamoja na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki na anayefuata ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungumza jambo na Balozi  Shelukindo baada ya kuapishwa.
Balozi Shelukindo (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wenzake kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.