Follow by Email

Wednesday, October 1, 2014

Ujumbe kutoka Marekani wataembelea Wizara ya Mambo ya NjeKaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (katikati) akizungumza na ujumbe wa wafanyabiashara na Mabalozi wa Heshima wa Tanzania nchini Marekani uliokuja kumtembelea Ofisini kwake. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TANAS Energy Group ya Marekani, Bw. William Crawford wa kwanza kulia kwa Kaimu Katibu Mkuu upo nchini kwa madhumuni ya kuangalia fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii. 
Ujumbe wa Marekani ukimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu hayupo pichani. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TANAS Energy Group ya Marekani, Bw. William Crawford, Balozi wa Heshima wa Tanzania, California, Bw. Ahmed Issa;  Rais wa Automated Transmission Rebuilding California, Bw.  Steve Horgan; Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Seafarers inc, Bibi Deborah Owens; na  Rais na Mwanzilishi wa Shirika la Women Empowered to Achieve the Impossible (WETATI), Bibi Margret Dureke,
Ujumbe mwingine ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kulia ni Mhandisi wa Tiba, San Francisco, California, Bw. Robert Reynolds; Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Bw. Suleiman Saleh; Bw. Andy Math na Balozi wa Heshima wa Tanzania, Michigan, Bw. Robert Shumake.


Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Gamaha akiagana na Kiongozi wa Msafara, Bw. William Crawford.

Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.