Follow by Email

Monday, October 27, 2014

Rais Kikwete atembelea Shirika la Simu la VIETTEL, Hanoi Vietnam

Wafanyakazi wa Shirika la Simu la VIETTEL wakiwa wamejipanga tayari kumpokea Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania muda mfupi kabla ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Hanoi, Vietnam Jumatatu Oktoba 27, 2014 Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Rais Kikwete kwenye mazungumzo na viongozi wa shirika hilo la simu linalomilikiwa na Serikali ya Vietnam. Kutoka kushoto ni Mhe. Lt. Gen. (Mstaafu) Abdurahman Shimbo, Balozi wa Tanzania nchini China na Vietnam; Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Katibu Mkuu Hazina Bw. Servicius Likwelile.

Mhe. Musa Azzan Zungu, Mbunge na pia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge akijitambulisha wakati wa maongezi rasmi baina ya ujumbe wa Rais Kikwete na viongozi wa Shirika la VIETTEL.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.