Follow by Email

Wednesday, October 1, 2014

Maafisa Wakuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini watembelea Wizara ya Mambo ya NjeKaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Joachim Otaru akitoa hotuba kuhusu Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, nafasi ya Tanzania katika kutekeleza majukumu ya kimataifa na uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kwa Maafisa Wakuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini. Maafisa hao wapo nchini kwa ziara ya mafunzo hadi tarehe 02 Oktoba 2014. 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent mwenye tai nyekundu akifafanua jambo kwa maafisa hao kuhusu nafasi ya Tanzania katika Jumuiya za Kikanda (SADC, EAC na ICGLR). Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko.

Bw. Shiyo akiendelea na ufafanuzi wa masuala mbalimbali.


Bw. Maleko akitoa neno la shukrani kwa maafisa wa Chuo hicho kwa uamuzi wao wa kuitembelea Wizara ya Mambo ya Nje. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.