Follow by Email

Wednesday, September 17, 2014

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje akutana na Balozi wa Tanzania Paris, Ufaransa

Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Mhe. Begum Taj, Balozi wa Tanzania Paris Ufaransa mara baada ya kuwasili Paris, Ufaransa leo tarehe 17 Septemba 2014.
Waziri Membe akiwa kwenye mazungumzo na mwakilishi wa kampuni ya Airbus Bw. Pierre-Etienne Courage. Akiwa Mjini Paris, Waziri Membe pia alikutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Kampuni ya Renault. Pia alipokea taarifa ya maendeleo ya ununuzi wa jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania nchini humo kutoka kwa Balozi Taj. Baada ya mikutano hiyo Mhe. Membe alielekea nchini Marekani kuhudhuria mikutano ya Umoja wa Mataifa. Wengine pichani ni maafisa wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje James Bwana na Olivia Maboko. Upande wa kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ulaya na Marekani Mama Vicky Mwakasege na Balozi Begum Taji.No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.