Follow by Email

Thursday, September 11, 2014

Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini

Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Mark Childress alipofika Wizarani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na kukumbuka Wahanga wa tukio la kigaidi lililotokea Marekani miaka 13 iliyopita (September 11th, 2001). Mazungumzo yao yalifanyika tarehe 11 Septemba 2014.
Mhe. Membe akimweleza jambo Balozi Childress wakati wa mazungumzo yao.
Balozi Childress pamoja na Bw. Vincent Spera, Afisa kutoka  Ubalozi wa Marekani wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.