Follow by Email

Wednesday, September 10, 2014

Rais Museveni awasili nchini kwa ziara rasmi ya siku moja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara rasmi ya siku moja.

Mhe. Museveni akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Museveni akisaliamiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Ladislaus Komba wakati wa mapokezi yake.
Mhe. Museveni akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala alipowasili Jijini Dar es Salaam kwa ziara rasmi ya siku moja.
Mhe. Rais Kikwete akiongozana na Mhe. Rais Museveni.
Mhe. Museveni akipita katikati ya Gwaride Maalum mara baada ya kuwasili nchini kwa ziara rasmi ya siku moja huku akisindikizwa na Mhe. Rais Kikwete.
Mhe. Rais Museveni kwa pamoja na Mhe. Kikwete wakiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa uwanjani hapo na kikundi cha matarumbeta wakati wa mapokezi.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Rais Museveni, Ikulu
Mhe. Rais Kikwete wakiwa katika chumba cha mazungumzo na Mhe. Rais Museveni.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.