Follow by Email

Wednesday, September 3, 2014

Naibu katibu Mkuu ashiriki hafla ya miaka 69 ya Taifa la Vietnam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akisoma hotuba wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba, 2014 na kuhudhuriwa na Mabalozi  wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wageni waalikwa.
Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vo Thanh Nam (kushoto) akiwa na Balozi wa Cuba nchini. Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (wa tatu kushoto) pamoja na Bi. Samira Diria (wa kwanza kulia), Afisa Mambo ya Nje wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam.
Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Zakaria Anshar (kushoto) akiwa na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Vietnam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam.
Sehemu ya Wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza Balozi Gahama akihutubia wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 69 ya Taifa la Vietnam iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Kaimu Murugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya akimpongeza Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vo Thanh Nam kwa miaka 69 ya uhuru wa taifa lake.

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.