Follow by Email

Friday, September 19, 2014

Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Dubai atembelea Wizara ya Maliasili na Utalii

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi Maimuna Tarishi akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai, Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah alipowasili Wizarani hapo na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi katika Wizara hiyo, Mhe. Lootah katika mazungumzo yake aligusia suala zima la utunzaji vivutio vya utalii na uboreshaji wa miundombinu kwa lengo la kukuza sekta ya Utalii.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akisalimiana na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Mhe. Omar Mjenga 
Bi. Maimuna Tarishi akielezea juu ya vivutio mbalimbali vilivyopo nchini na sifa za vivutio hivyo katika mazungumzo na Mhe. Lootah pamoja na ujumbe alioambata nao pia aliwahamasisha Dubai kuja kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Utalii 
Mazungumzo yakiendelea
Kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw Iddi Mfunda  akichangia katika mazungumzo.
Balozi Mdogo,  Omar Mjenga akichangia jambo katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Wizara ya Maliasili na Utalii
Mhe. Lootah akichangia jambo wakati wa mazungumzo huku wajumbe wengine wakimsikiliza


Picha ya pamojaReginald PhilipNo comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.