Follow by Email

Monday, September 1, 2014

Mhe. Omar Mjenga akutana na Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce

Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai Mhe. Omar Mjenga akutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry.
-----------------------------------------------------------------------


Mhe. Omar Mjenga, amekutana na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry na kufanya naye mazungumzo.

Katika mazungumzo, wamejadiliana uwezekano wa kuwa na ziara ya kibiashara kwenda Tanzania, kwa makampuni na viwanda vilivyopo Dubai, ili kukutana na wafantabiashara na wamilikiwa viwanda Tanzania, ilikujionea na kuibua furs za uwekezaji. Wamekubaliana ziara hiyo ifanyike mwanzoni mwa mwaka kesho na hivyo basi kuanza maandalizi mapema
Mwezi Novemba, kutakuwa na ziara ya kibiashara ya makampuni kutoka Flame ya Ajman.

Aidha, wamezungumzia kuhusu mkutano wa Africa Global Business Forum utakaofanyika tarehe 1 - 2 Oktoba 2014 hapa Dubai.
Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum amemwalika Rais Kikwete kuhudhuria pamoja na marais wengine wa Mali, Ghana, Uganda, Mozambique, Ethiopia, Senegal, Burkina Faso, Sudan na Ivory Coast.

Mkutano huu hufanyika kila mwaka ambao huzungumzia njia muafaka wa ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na UAE kwa ujumla na nchi za Afrika.No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.