Follow by Email

Friday, September 19, 2014

Makamu wa Rais akutana kwa mazungumzo na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Dubai

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la  Dubai, Mhe. Ali Rashid Ahmed Lootah alipofika   Ofisi kwake kumsalimia na kufanya nae mazungumzo. Mhe. Lootah alimwelezea Makamu wa Rais dhumuni la ziara yake nchini Tanzania kuwa ni kuangalia nafasi ya uwekezaji katika Sekta ya Utalii, Ujenzi wa Nyumba na Makazi ya watu.
Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la  Dubai, Mhe. Lootah akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Makamu wa Rais
Mhe. Dkt. Bilal akizungumza na Mhe. Lootah
Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Bilal akimsikiliza Mhe. Lootah alipokuwa akizungumza naye Ofisini kwake. Kulia kwa Mhe. Dkt. Bilal ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya.

Mazungumzo yakiendelea.
Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Gharib Bilal akiagana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai  mara baada ya mazungumzo yao
Wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.