Follow by Email

Sunday, August 10, 2014

Balozi Chabaka afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Exim Bank

Mhe. Chabaka Kilumanga (wa pili kushoto), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mazungumzo na Bw. Yogesh Manek, Mwenyekiti wa Bodi ya Exim Bank, kwenye Makazi ya Balozi, mjini Moroni. Maudhui ya mazungumzo hayo yalihusu azma ya Ubalozi ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Comoro kwa lengo la kuwezesha kila upande kutambua wafanyabiasha wanaotambulika na kuaminika  na pia kuwahamasisha kufanya biashara kwa kutumia taratibu rasmi. Uongozi wa Exim Bank umekubali kusaidia kifanyanikisha azma hiyo. Mhe. Balozi na Bw. Manek walizungumzia pia uwezekano wa Exim Bank kudhamini mradi mkubwa wa umeme ambao unategemewa kuanzishwa kati ya Shirika la Umeme la Comoro na Kampuni ya DACC Global ya Marekani kwa kushirikiana na Kampuni ya NSI Energy ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.