Follow by Email

Thursday, July 24, 2014

Wizara yamuaga Balozi wa Norway nchini


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernad K. Membe (Mb.) kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Norway nchini, Mhe. Ingunn Klepsvik ambaye amemaliza muda wake wa kazi. Hafla hiyo fupi ya chakula cha mchana ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam.
Balozi Mushy akimkabidhi Balozi Klepsvik zawadi ya picha ya kuchora ya Twiga  kama ukumbusho wake kwa Tanzania
Balozi Klepsvik naye akizungumza machache wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mabalozi  ambaye pia ni Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (kushoto) pamoja na Balozi Mushy na Balozi Klepsvik wakati wa hafla hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi Victoria Mwakasege akiwakaribisha wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Klepsvik.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.