Follow by Email

Monday, July 28, 2014

Naibu Waziri akutana na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za AtomikiNaibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.)  akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Kimatifa la Nguvu za Atomiki,  Bw. Yukiya Amano alipofika Wizarani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Shirika lake na Serikali ya Tanzania. Bw. Amano yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Mahadhi akizungumza na Bw. Amano
Mhe. January Makamba (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia pamoja na Wajumbe wengine akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero (wa pili kulia) na Msaidizi wa Mhe. Maalim, Bw. Adam Isara (kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Maalim na Bw. Amano (hawapo pichani). 
Bw. Amano akimweleza jambo Mhe. Maalim wakati wa mazungumzo yao.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakifuatilia mazungumzo.
Wajumbe wengine.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Japhet Mwaisupule na Bi. Ramla Khamis, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo.


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.