Follow by Email

Friday, July 18, 2014

Naibu Katibu Mkuu amuaga Balozi wa Israel nchini

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Gil Haskel, Balozi wa Israel nchini Tanzania ambaye alifika Wizarani kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake. Kwenye mazungumzo yao, Balozi Gamaha ameishukuru Serikali ya Israel kwa ushirikiano mzuri na Serikali ya Tanzania hususan kwenye upande wa kujengea uwezo wa Watanzania kwenye masuala ya Kilimo cha Umwagiliaji. Kwa upande wake Balozi Haskel ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa alioupata katika kipindi chake. Pia ameahidi kuendeleza ushirikiano huo hata katika wadhifa wake mpya akiwa nchini kwake, ambapo atakua Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Israel.

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati,  Balozi Simba Yahya (kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Bw. Leonce Bilauri, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia na kunukuu mazungumzo kati ya Naibu Kaibu Mkuu na Balozi wa Israel nchini.

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.