Follow by Email

Thursday, July 3, 2014

Mwanamfalme Akishino wa Japan awasili nchini kwa ziara rasmi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Mwanamfalme Akishino wa Japan mara baada ya Mwanamfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku tano hapa nchini.
Mhe. Mahadhi na Mwanamfalme Akishino wa Japan wakiendelea na mazungumzo huku Mke wa Mwanamfalme huyo (kulia) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Salome Sijaona (kushoto) na Balozi wa Japan hapa nchini, Mhe.  Masaki Okada wakisikiliza.
Mazungumzo yakiendelea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.