Follow by Email

Wednesday, July 16, 2014

Mhe. Rais apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa New Zealand hapa nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mhe. Richard Stuart Mann, Balozi wa New Zealand hapa nchini mwenye makazi yake Afrika Kusini. Hafla hiyo fupi ilifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai, 2014.

Balozi Mann akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya Balozi huyo kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete, wakwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi maalum Mhe. Prof. Mark J. Mwandosya (Mb.)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Richard Stuart Mann
Balozi Richard Stuart Mann akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Balozi Mann akisikiliza Wimbo wa Taifa lake ukipigwa kwa heshima yake mara baada ya kuwasili Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage na wakwanza kushoto ni Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo


Picha na Reginald PhilipNo comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.