Follow by Email

Monday, June 30, 2014

Mhe. Membe amuaga rasmi Balozi wa Afrika Kusini nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thanduyise Henry Chiliza ambaye amemaliza muda wake wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) Jijini Dar es  Salaam.
Balozi Chiliza (kulia) akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (katikati) pamoja na Balozi wa Nigeria hapa nchini, wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Chiliza.
Balozi Chiliza nae akizungumza 
Mhe. Membe na Balozi Chiliza wakigonganisha glasi kutakiana afya njema na ushirikiano imara kati ya Tanzania na Afrika Kusini
Mhe. Membe akimkabidhi Balozi Chiliza zawadi ya picha ya kuchora ya Mlima Kilimanjaro.
Picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.