Follow by Email

Sunday, June 22, 2014

Makamu wa Rais wa China awasili nchini kwa ziara ya kikaziMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimlaki kwa furaha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2014 kwa ajili ya kuanza rasmi ziara yake ya kikazi  ya siku tano hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju aliyekuwepo Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi ya Makamu huyo wa Rais.
Mhe. Li Yuanchao akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki mara baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa China Mhe. Li Yuanchao akipita  katikati ya Gwaride la Heshima wakati wa mapokezi yakehuku  akisindikizwa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt. Bilal.
Mhe. Li akifurahia kikundi cha burudani kilichokuwa uwanjani hapo (hawapo pichani) wakati wa mapokezi yake.
Moja ya vikundi vya burudani vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa China alipowasili hapa nchini.
Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.