Follow by Email

Friday, June 27, 2014

Makamu wa Rais wa China amaliza ziara yake nchini


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mohamed Gharib Bilal akiagana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao baada ya kukamilisha ziara yake ya siku sita hapa nchini. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Li alisaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na China pia alipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Zanzibar, Ngorongoro pamoja na kukabidhi gari la kurushia matangazo ya Televisheni  nje ya studio (OB Van) kwa Shirika la Utangazaji la Tanzanaia (TBC).
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Mhe. George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora kabla ya kuondoka nchini.
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Mhe. Fenella Mukangara (Mb.), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Philip Mangula
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Abdulrahman Shimbo.
Kikundi cha burudani kikitumbuiza wakati Mhe. Li akiondoka nchini.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.