Follow by Email

Wednesday, June 25, 2014

Matukio mbalimbali ya ziara ya Makamu wa Rais wa China Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akivalishwa shada la maua huku Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akishuhudia mara baada ya kuwasili  Mhe. Li kuwasili Zanzibar kwa ziara ya siku mbili Visiwani humo
Mhe. Li akisalimiana na  Mhe. Yusuph Mzee, Waziri wa Fedha wa Zanzibar pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliofika kumpokea.
Mhe. Li akisalimiana na Balozi Silima Haji, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar


Mhe. Li pamoja na Mawaziri  katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka China wanaotoa huduma katika Hospitali za Zanzibar
Mhe. Li na Mhe. Balozi Idd wakiwa wamewasili kwa ajili ya kuanza mazungumzo rasmi kuhusu ushirikiano kati ya Zanzibar na China.
Mhe. Balozi Idd akiwa na baadhi ya Mawaziri waliohudhuria mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa China (hayupo pichani)


Mhe. Li na baadhi ya wajumbe alifuatana nao katika mazungumzo na Mhe. Balozi Idd (hayupo pichani)
Mhe. Li na ujumbe wake wakati wa mazungumzo.
Mhe. Balozi Idd na ujumbe wake wakati wa mazungumzo na Mhe. Li  na ujumbe wake (hawapo pichani)
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo. Wa tatu kutoka kulia ni Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Li na Mhe. Balozi Idd wakishiriki hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa kwa heshima ya Makamu huyo wa Rais kutoka China

Mhe. Li akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Shamba la Viuongo vya Chakula huko Kizimbani Zanzibar
Mhe. Li akiangalia moja ya kiuongo aina ya manjano au tumeric alipotembelea shamba la viungo vya chakula huko Kizimbani Zanzibar. Anayempatia kiungo hicho ni Bw. Fumu Ali Garo.
Mhe. Li akiwaonesha kitu kwa mbali Wajumbe aliofuatana nao mara baada ya kutembelea eneo la kihistoria la Ngome Kongwe Zanzibar. Mwenye tai nyekundu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mhe. George Mkuchika.
Mhe. Li akipata maelezo kuhusu historia ya watawala wa kiarabu waliowahi kuitawala Zanzibar zamani kutoka kwa Mkurugenzi wa Makumbusho na Mambo ya Kale, Bi Amina Ameir.No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.