Follow by Email

Friday, May 30, 2014

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki ziarani nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimpokea kwa furaha Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Ahmet Dovutoglu ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu yenye lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki.
Mhe. Membe akiwa ameongozana na Mhe. Dovutoglu mara baada ya kumpokea wakielekea katika Hoteli ya Hyatt Regency kwa ajili ya mazungumzo rasmi.
Mhe. Membe na Mhe. Dovutoglu wakiwa na Wajumbe waliofuatana nao wakati wa mazungumzo rasmi.
Mhe. Membe kwa pamoja na Mhe. Dovutoglu wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuangalia namna Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linaweza kushirikiana na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) 
Mhe. Waziri Membe akizungumza.
Baadhi ya Wakurugenzi na Kaimu Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe. Dovutoglu nae akizungumza wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
Mkutano ukiendelea
Mhe. Membe kwa pamoja na Mhe. Dovutoglu wakijibu maswali ya waandishi wa habari.
Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.