Follow by Email

Wednesday, May 14, 2014

Mhe. Membe amuaga Marehemu Balozi Flossie nyumbani kwake Malawi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisoma kwa majonzi Salamu za Pole za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Marehemu Flossie Gomile-Chidyaonga. Mhe. Waziri Membe alisoma salamu hizo wakati wa kumuaga Marehemu Balozi Flossie tukio hilo lilifanyika nyumbani kwa marehemu Kitongoji cha Limbe katika mji wa Blantyre nchini Malawi. Mhe. Membe alimwakilisha Rais Kikwete kwenye mazishi ya Balozi Flossie yaliyofanyika tarehe 14 Mei, 2014.
Mhe. Membe akiendelea kusoma salamu hizo huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Ephraim Chiume (mwanye tai nyeusi) na Mume wa Rais wa Malawi, Jaji Mkuu Mstaafu, Banda (wa kwanza kulia mstari wa kwanza) wakimsikiliza.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Chiume Salamu hizo mara baada ya kuzisoma.
Mhe. Chiume nae akisema machache wakati wa shughuli za kumuaga Balozi Flossie. Katika maelezo yake Mhe. Chiume kwa niaba ya Serikali ya Malawi alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa wakati wote wa msiba wa Marehemu Balozi Flossie.
Mhe. Chiume akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe waliofuatana na Mhe. Membe nchini Malawi.
Baba Mdogo wa Marehemu Balozi Flossie, Dkt. Joseph Gomile nae akitoa neno wakati wa shughuli hizo za kumuaga Marehemu Balozi Flossie. Dkt. Gomile ambaye   anaishi nchini Tanzania kwa kipindi kirefu sasa nae aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa mchango mkubwa katika msiba huo mzito wa mtoto wake.
Mhe. Membe. Mhe. Chiume na Mhe.  Jaji Mstaafu Banda wakimsikiliza Dkt. Gomile (hayupo pichani)
Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini waliomsindikiza mwenzao Marehemu Balozi Flossie nao wakifuatilia matukio.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Baloz Flossie kama linavyoonekana katika eneo la nyumbani kwake likiwa limezungukwa na waombolezaji.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. PatrickTsere  (kushoto)  akiwa na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Malawi hapa nchini mara baada ya shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Balozi Flossie kumalizika.
Baadhi ya viongozi wa dini waliokuwepo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki kumuaga Balozi Flossie katika eneo la nyumbani kwake kabla ya mazishi.
Marafiki wa Marehemu Balozi Flossie wakiwa katika simanzi kufuatia kifo cha mpendwa wao.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mabalozi aliofuatana nao nchini Malawi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.