Follow by Email

Monday, May 19, 2014

Mfanyakazi Hodari wa Wizara na Wafanyakazi Bora wapokea vyeti vyao

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Dushhood Mndeme akijiandaa kutaja majina ya Wafanyakazi Bora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwemo Mfanyakazi Hodari  wakati wa Kikao cha 8 cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Waliokaa ni Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. John Haule (mwenye miwani), Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (wa kwanza kulia), Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Cosato Chumi (mwenye tai nyekundu) na Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi na Bi. Asya Hamdani.
Baadhi ya Wafanyakazi Bora wakiwa na nyuso za furaha.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Bw. Haule akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Hodari wa Wizara Bw. Bujiku Sakila kutoka Idara ya Afrika.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Ally Kondo.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bi. Asya Hamdani.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Sera na Mipango,  Bw. Elly Chuma.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya DIASPORA, Bw. Seif Kamtunda.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Ibrahim Mamboya.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Gloria Mboya.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Batholomeo Jungu.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rose Kitandula.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi wa Kada ya Makatibu Muhtasi , Bi. Faith Masaka.
Katibu Mkuu akimkabidhi Cheti Mfanyakazi Bora wa Kada ya Wahudumu, Bi. Hadija Mwichande.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia tukio la utoaji vyeti kwa Wafanayakazi Bora wa Wizara
Bw. Iman Njalikai, Mwenyekiti wa TUGHE wa Wizara akizungumza mara baada ya utoaji vyeti kwa Wafanyakazi Bora wa Wizara.

Katibu Mkuu akibadilishana neno na baadhi ya Wajumbe mara baada ya kikao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.