Follow by Email

Saturday, May 24, 2014

Maadmisho ya Siku ya Afrika kufanyika Jumapili


Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vicent Kibwana akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari kuelezea maadhimisho ya Siku ya Afrika yatakayofanyika katika Viwanja vya Karimjee siku ya Jumapili tarehe 25 Mei, 2014. wengine katika picha ni Mhe. Meja Gen. Edzai Chimonyo (kushoto), Kaimu Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrrika ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania na Balozi wa DRC nchini Tanzania, Mhe. Juma Mpango (kulia). kaulimbiu ya mwaka huu ya siku ya Afrika ni Kilimo na Usalama wa Chakula ambapo Waheshimiwa Mabalozi walisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kutoa kipaumbele katika sekta ya kilimo kwa kutengeneza sera nzuri za umiliki wa ardhi ili itumike kama dhamana katika taasisi za fedha. 

Balozi wa kenya nchini Tanzania akichangia mada kuhusu kaulimbiu ya Siku ya Afrika.

Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini Tanzania na wana habari wakiendelea na mkutano.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.