Follow by Email

Wednesday, March 12, 2014

Katibu Mkuu amkabidhi Hati za kazi Mwakilishi wa Heshima wa Mauritius hapa nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkabidhi  Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi Hati zinazomwezesha kufanya kazi kama Mwakilishi wa Heshima wa Mauritius nchini Tanzania. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Katibu Mkuu tarehe 12 Machi, 2014. 
Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kupokea kibali cha kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Mauritius hapa nchini
Katibu Mkuu,  Bw.  Haule akizungumza na  Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akiagana na Bw. Syed Nazre Abbas Rizvi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.