Follow by Email

Saturday, January 11, 2014

Rais Kikwete awaandalia Mabalozi Sherehe ya kuukaribisha mwaka 2014Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akihutubia Mabalozi na wawakilishi wa taasisi za kimataifa wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia Ikulu, jana jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) (kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

 
Mhe. Balozi Juma Mpango, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye pia ni Kiongozi wa Mabalozi hapa nchini, wakati akihutubia katika sherehe hiyo.   

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa wanawake wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia jana. 

Rais Kikwete (wa saba kulia, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (wa sita kulia, mstari wa mbele), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) (wa sita kushoto, mstari wa mbele), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pamoja na Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa wakati wa Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya (Sherry Party) aliyowaandalia jana Ikulu. 


Picha zote na maelezo kwa hisani ya Michuzi Blog 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.