Follow by Email

Wednesday, December 11, 2013

Malkia Maxima wa Uholanzi awasili nchini


 
Malkia  Maxima wa Uholanzi akiwa amefuatana na Mwenyeji wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Mwingine pembeni ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Raymond Mushi.

Malkia Maxima kwa pamoja na Mhe. Mama Salma wakifurahia burudani kutoka kwa mojawapo ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani wakati wa mapokezi.
 
Wakuu wa Wilaya za Kinondoni na Temeke, Mhe. Jordan Rugimbana (wa nne kutoka kushoto) na Mhe. Sophia Mjema (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima. Wengine ni Balozi Dora Msechu (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika na Bw. Songelaeli Shila, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Mama Salma akimtambulisha kwa Malkia Maxima  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Ne na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu. Pembeni kwa Balozi Msechu ni Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika.

Malkia Maxima kwa pamoja na Mama Salma wakifurahia  wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Bi. Ertharin Cousin akiwaeleza jambo mara baada ya Malkia Maxima kuwasili nchini.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou (kushoto) akiwaeleza jambo Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Wilson Masilingi (katikati)  na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe. Jaap Frederics wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima wa Uholanzi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.