Follow by Email

Tuesday, November 26, 2013

Tanzania na Umoja wa Mataifa zasaini Mkataba wa Uenyeji wa kujenga taasisi ya kuhifadhi nyaraka za Mahakama ya ICTR

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kulia na Mwanasheria kutoka Umoja wa Mataifa, Bw.Serpa Soares wakiweka saini Mkataba ambapo Tanzania itakuwa Mwenyeji wa Taasisi mpya ya Umoja wa Mataifa itakayojengwa mjini Arusha kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda. Uwekaji saini huo ulifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam tarehe 26 Novemba, 2013.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), (kulia) akibadilishana mikataba na Bw. Soares mara baada ya shughuli ya uwekaji saini kukamilika.

Kutoka kushoto ni Balozi Dora Msechu, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Lugaganya, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bibi Naomi Zegezege, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria na Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje wakishuhudia uwekaji saini huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Bw. Soares mara baada ya kukamilisha shughuli za uwekaji saini. katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri alilishukuru Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa taasisi itakayohifadhi kumbukumbu na nyaraka za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda.


Mazungumzo yakiendelea huku ujumbe wa Tanzania uliokaa upande wa kulia na ujumbe wa Umoja wa Mataifa ukifuatilia mazungumzo hayo.

Bw. Soares akisisitiza jambo huku Mhe. Membe akisikiliza kwa makini. wengine katika picha ni ujumbe wa Tanzania uliokaa upande wa kulia na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokaa upande wa kushoto.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiagana na Bw. Soares mara baada ya shuguli ya uwekaji saini kukamilika

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.