Follow by Email

Thursday, November 14, 2013

Mkutano wa Ngazi ya Maafisa Waandamizi wa Afro Arab Summit wafunguliwa

Hii ni Meza Kuu wakati wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Ushirikiano baina ya Nchi za Afrika na Kiarabu {Afro Arab Summit} ulioanza tarehe 14 Novemba, 2013 nchini Kuwait

Mwenyekiti wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi ambayre pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait akitoa hotuba ya ufunguzi. Alisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika na Kiarabu kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi,hususan katika uwekezaji na biashara

Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania, Dkt. Uledi Juma Mussa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara akisikiliza kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa mkutano

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini mkutano. kutoka kulia, Mhe. Balozi Simba Yahya, Mkurugnzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, anayefuata, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia ambaye pia anashughulikia masuala ya Afro Arab na Mhe. Prof. Abdillah Omar, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ambaye anawakilisha pia Kuwait na Qatar.

Sehemu ya ujumbe katika ukumbi wa mkutano

baadhi ya bendera katika ukumbi wa mkutano

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.