Follow by Email

Monday, November 18, 2013

Dkt. Bilal kuongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Afro Arab Summit

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal akiongea na ujumbe wake {haupo pichani}wakati wa kikao cha maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa Afro Arab Summit utakaofanyika nchini Kuwait tarehe 19 na 20 Novemba, 2013. kikao hicho kilifanyika katika moja ya kumbi za Jumba la Mfalme wa Kuwait.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe {Mb}, akitoa taarifa kwa Makamu wa Rais kuhusu masuala yatakayojadiliwa katika Mkutano wa Afro Arab Summit.


Mbunge wa Wawi, Mhe. Hamadi Rashidi naye akichangia jambo kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Afro Arab Summit. Aliyevaa kofia ni Mbunge wa Gando, Mhe. Khalifa Khalifa.

Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz akichangia hoja katika kikao hicho.

Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa sita kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake katika mkutano wa Afro Arab Summit.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.