Follow by Email

Thursday, November 7, 2013

Balozi Kasyanju akutana na Msimamizi wa Mahakama mbadala ya ICTR


Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akisalimiana na Bw. Samuel Akorimo, Afisa Msimamizi wa Mahakama iliyorithi shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ya mjini Arusha. Bw. Akorimo alifika Wizarani kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mahakama hiyo na Wizara. Wanaoshuhudia ni Bw. Tiyarijana Mphepo, Afisa alifyefuatana na Bw. Akorimo na Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje.

Bw. Akorimo akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Wizarani huku Bw. Mphepo akishuhudia.


Bw. Akorimo akizungumza na Balozi Kasyanju  kuhusu majukumu ya Mahakama hiyo.

Balozi Kasyanju akizungumza na  Bw. Akorimo huku Maafisa wakinukuu mazungumzo hayo.

 
 
Picha na Reginald Philip 
 
 
No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.