Follow by Email

Wednesday, November 6, 2013

Balozi Kamala ateuliwa kuwa Mjumbe wa Troika ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific (ACP)


 
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya, Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akizungumza na Balozi wa Sudan Jumuiya ya Ulaya Mhe. Fidail Eltigani.  Balozi Eltigani alifika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya – Brussels kumweleza Mhe. Balozi Kamala kuhusu uamuzi wa Mabalozi wa ACP kanda ya mashariki wa kumteua kuingia kwenye Troika ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific.  Balozi Kamala atakaa kwenye Troika kwa kipindi cha miezi kumi na nane (18) na kuanzia Januari 2014 atakuwa mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific – Brussels. No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.