Follow by Email

Friday, September 20, 2013

Waziri Membe akiwa na Mabalozi wa Heshima


Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Heshima Kjell Bergh kutoka Minnesota wakitia saini mkataba wa Ubalozi wa Heshima huku Afisa Paul Mwafongo (kushoto) na Afisa Suleiman Saleh (watatu toka kushoto) wakiwaelekeza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akimkabidhi mkataba mmoja wa Mabalozi wa Heshima Kjell Bergh kutoka Minnesota.
 

 Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Heshima Hon. Charles Gray kutoka Pennsylvania wakitia saiini mkataba wa Ubalozi wa Heshima huku wakisaidiwa na Afisa Paul Mwafongo na Suleiman Saleh.


Mhe. Waziri Membe akiongea machache mara baada ya zoezi zima la utiaji saini wa Mabalozi wa Heshima kukamilika.  Kulia ni Afisa wa Habari wa Ubalozi Mindi Kasiga, ambaye alikuwa mshereheshaji wa hafla hiyo.
Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb) (watatu kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Heshima nchini Marekani.  Wengine katika picha ni Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa nne kulia), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na Balozi Dora Msechu (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Picha na maelezo kutoka Vijimambo blog


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.