Follow by Email

Friday, September 13, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) amemteua Brigedia Jenerali Mstaafu, Balozi Francis Mndolwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Balozi Mndolwa ameteuliwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi hivi karibuni. 

Brigedia Jenerali Mstaafu Mndolwa aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi kabla ya kustaafu utumishi wa umma.

Uteuzi wa Balozi Mndolwa unaanza mara moja.


Imetolewa na: 

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, 

DAR ES SALAAM

12 SEPTEMBA, 2013.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.