Follow by Email

Monday, September 23, 2013

Mhe. Membe akutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimsikiliza  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Kamalesh Sharma walipokutana mjini New York kwa mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya hiyo, ikiwemo maandalizi ya Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchi na Serikali (CHOGM)  unaotarajiwa kufanyika nchini Sri Lanka mwezi Novemba, 2013. Mhe. Membe yupo mjini New York kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68  cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Membe akimsikiliza Mhe. Sharma wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Maafisa walioambatana na Mhe. Sharma, Balozi Adonia Ayebare (kushoto) pamoja na Msaidizi wa Waziri, Bw. Togolani Mavura.
Mhe. Waziri  akisoma barua aliyokabidhiwa na Mhe. Sharma walipokutana.
Mmoja wa Maafisa waliofuatana na Mhe. Sharma akifafanua jambo wakati wa mazungumzo.

Mhe. Membe akisisitiza jambo wakati akiagana na Mhe. Sharma mara baada ya mazungumzo yao.
Mhe. Membe akifurahia jambo na wageni wake kabla ya kuagana nao .


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.