Follow by Email

Wednesday, September 11, 2013

Maonesho ya bidhaa za China yafunguliwa Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb) akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya China - Africa Show yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam tarehe 10 Septemba, 2013.


Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. LV Youqing naye akitoa hotuba katika maonesho hayo


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda (Mb) akitoa neno la kumkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia watu waliohudhuria ufunguzi wa maonesho ya China - Africa Show.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia), Bw Omar Mjenga na Bw. Mkumbwa Ally, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje wa tatu kutoka kulia wakisikiliza kwa makini hotuba zinazotolewa na viongozi mbalimbali


Baadhi ya watu waliohudhuria ufunguzi huo. Mstari wa mbele ni viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania na ya China akiwemo Mhe. Waziri Mkuu wa tano kutoka kulia.


Mhe. Mizengo Peter Pinda wa nne kutoka kulia akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa maonesho hayo


Mhe. Waziri Mkuu akiangalia mfano wa nyumba ya kisasa baada ya kufungua maonesho hayo.


Mhe. Waziri Mkuu akiangalia zana mbalimbali kama vile matrekta na majenereta
Picha na Reginald Philp KisakaNo comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.