Follow by Email

Tuesday, September 24, 2013

ASKARI WA JWTZ ALIYEJERUHIWA CONGO NA KUFARIKI AAGWA LEO LUGALO


Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza

Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Askari mwenzao, Marehemu Private, Hugo Munga alifariki dunia Septemba 18 mwaka huu huko Pretoria Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata akiwa na vikosi vya MONUSCO Congo DRC katika operations ya kuwaondoa waasi wa M23. Mwili wa Munga ulisafirishwa jana kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu ilifanyika Viwanja vya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam.

Wanajeshi wa JWTZ waliokuja kumuaga Mwanajeshi mwenzao Marehemu Jovitha Barnaba Munga.


Mama wa Marehemu, Jovitha Barnaba Munga akisaidiwa kuaga mwili wa mwanae.

Baadhi ya waombolezaji ambao ni Askari wenzake Marehemu pamoja na wana familia wakiwa eneo la tukio.

Wanajeshi wa JWTZ wakipita kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu.

Picha na maelezo kwa hisani ya Father Kidevu blog
No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.