Follow by Email

Thursday, August 22, 2013

Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Kenya

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Mutinda Mutiso akitembea sambamba na Bibi Zuhura Bundala. Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wakati alipokuwa anaingia kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro kwa ajili ya hafla ya kumuaga.
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kushoto akisalimiana na Balozi wa Kenya kabla ya kuanza kwa hafla ya kumuaga.
 

Mhe. Waziri akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency.
 

Bibi Bundala akitoa neno kwa ajili ya kumkaribisha Mhe. Waziri kutoa hotuba ya kumuaga Balozi wa Kenya.
 

Mhe. Membe akitoa hotuba ambayo ilisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya Tanzania na Kenya.
 

Balozi wa Kenya anayemaliza muda wake akitoa hotuba ambapo alishukuru kwa ushirikiano aliopata kutoka Serikali ya Tanzania uliomwezesha kutekeleza majukumu yake kwa wepesi.
 

picha ya pamoja
Picha na Reginald Kisaka

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.