Follow by Email

Thursday, August 1, 2013

Waziri Mkuu wa Thailand aondoka baada ya kukamilisha ziara ya siku tatu nchini

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Thailand, Mhe. Yingluck Shinawatra wakisikiliza nyimbo za mataifa yao zilipopigwa kuashiria mwisho wa ziara ya Mhe. Shinawatra hapa nchini. 

Mhe. Rais Kikwete akimsindikiza Mhe. Shinawatra kuelekea kwenye ndege mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu hapa nchini.

Mhe. Shinawatra akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki pamoja na Mhe. Mary Nagu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji kabla ya kuondoka nchini baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu.

Mhe. Shinawatra akipunga mkono kuagana na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani) na  Viongozi wengine waliofika kumuaga mara baada ya kukamilisha ziara yake.

Mhe. Nagu na Viongozi wengine waliofika Uwanjani kumuaga Waziri Mkuu wa Thailand.


Mhe. Rais Kikwete na Viongozi wengine wakipunga mkono kumuaga Waziri Mkuu wa Thailand

Ndege iliyombeba Waziri Mkuu wa Thailand ikiondoka kuashiria kukamilika kwa ziara ya siku tatu ya kiongozi huyo hapa nchini.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.