Follow by Email

Wednesday, August 7, 2013

Waziri Membe afuturisha Watumishi wa WizaraMhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwakaribisha wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mufti Mkuu wa Tanzania na Wafanyakazi wa Wizara ya Mamob ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Futari Maalum aliyowaandalia nyumbani kwake jana, jijini Dar es Salaam. 


Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe. 

Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Waziri. Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb) (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimsikiliza Mhe. Waziri.  Katika picha pia ni Bw. James Lugaganya (kulia), Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa.  

Mhe. Waziri Membe akimsikiliza Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Simba. 

Mhe. Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Algeria na Omani hapa nchini. 

Mhe. Naibu Waziri akiwa anachukua Futari tayari kwa ajili ya kufuturu. 

Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa naye akishiriki katika Futari hiyo.

Wageni mbalimbali katika Futari ilyoandaliwa nyumbani kwa Mhe. Waziri Membe.

Akina mama nao wakijumuika katika kuchukua Futari tayari kwa ajili ya kufuturu. 

Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifurahia Futari hiyo.

Wafanyakazi wa Wizara wakiwa mezani wakifuturu. 

Mama Dorcas Membe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliohudhuria Futari. 

Mama Dorcas Membe akiteta jambo na mmoja wa wageni. 


Mhe. Waziri Membe akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu John Haule (kulia) na Naibu Katibu Mkuu Balozi Rajabu Gamaha wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimuaga Balozi Maharage Juma, Mkuu wa Itifaki.   

Baadhi ya Mashekhe wakisoma dua. 

Mhe. Waziri Membe akiagana na Mhe. Balozi Yahya bin Mosa al Bakri wa Oman nchini. 

Mhe. Waziri Membe akiagana na Mhe. Balozi Hossam Moharam wa Egypt hapa nchini. 

Waziri Membe akiagana na Mhe. Balozi Djelloul Tabet wa Algeria nchini. 

Waziri Membe akiagana na Balozi wa Iran hapa nchini. 

Mhe. Waziri Membe akiteta jambo na Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Mhe. Waziri Membe akiteta jambo na Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Waziri Membe akiteta jambo na Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Waziri Membe akifurahia jambo na Bw. Omari Mjenga, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Waziri Membe akiagana na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.