Follow by Email

Tuesday, August 20, 2013

Kikao cha Uongozi wa Wizara na Kamati ya Bunge chafanyika


Mhe. Edward Lowassa (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Mbunge wa Monduli akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika  Ofisi Ndogo za Bunge tarehe 19 Agosti, 2013.

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwasilisha  Taarifa ya Wizara ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge (hawapo pichani).
Baadhi ya Waheshimiwa wa Wabunge ambao pia  ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).

Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa karibu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Membe (hayupo pichani).

Kikao kikiendelea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.